Marehemu Kambi enzi za uhai wake.
HATARI! Wimbi la mauaji yanayohusishwa na matukio ya
mafumanizi yanazidi kushika kasi mkoani hapa ambapo mwishoni mwa wiki
iliyopita dereva mwingine wa bodaboda aliyetajwa kwa jina moja la Kambi
(33), anadaiwa kuchinjwa na kufa papohapo huku kifo chake kikihusishwa
na matukio hayo...
Tukio hilo lilitokea juzikati majira ya saa 11:00 alfajiri ambapo
mwili wa bodaboda huyo uliokotwa maeneo ya Modeko jirani na Makutano ya
Barabara za lringa na Mazimbu na kusababisha mkewe kuchanganyikiwa huku
ndugu wakiwa hawaamini.
Mke wa marehemu akiwa mwenye huzuni kubwa.
Muda mfupi baada ya tukio hilo, mwanahabari wetu alifika eneo la
tukio na kuushuhudia mwili wa jamaa huyo ukiwa umetupwa lakini
hawakuchukua chochote kutoka kwa marehemu huku wakimwachia bodaboda yake
na waleti ikiwa na fedha taslimu shilingi laki 240,000.
Ndugu wa marehemu Kambi.
Kufuatia hali hiyo baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo, walidai
huenda jamaa huyo alifumaniwa na mke wa mtu kwani mara ya mwisho
alionekana akiwa amempakiza mwanamke hivyo kuna madai kwamba mwenye mali
hakuwa na sababu ya kuchukua chochote zaidi ya kumtoa roho.Majira ya
saa 12:00 asubuhi, polisi walifika eneo hilo la tukio na kuuchukua mwili
wa marehemu na kuupeleka mochwari kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Morogoro.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Leonard Paul.
Baada ya tukio hilo, mwanahabari wetu kusaka undani wa kifo cha
bodaboda huyo. Kwenye eneo la tukio, ilidaiwa kwamba jamaa huyo aliuawa
katika tukio lililohusisha fumanizi la mke wa mtu kwani baada ishu hiyo
wahusika walitoka nduki bila kuchukua Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Morogoro, SACP Leonard Paul alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo.
No comments:
Post a Comment