Hosti wa Kipindi cha Wanawake Live kupita Televisheni ya EATV, Joyce Kiria.
WHY Joyce? Hosti wa Kipindi cha Wanawake Live kupita
Televisheni ya EATV...
Joyce Kiria yupo kwenye wakati mgumu baada ya
kukwaa skendo ya utapeli kwa marafiki zake (majina yanahifadhiwa kwa
sasa) akidaiwa kuwashawishi kuingia kwenye biashara ya Mtandao ya
Telexfree Network Marketing.
Kwa mujibu wa sosi makini, ishu hiyo imeibuka juzikati ambapo Joyce
alikuwa akishushiwa zigo la lawama na marafiki zake hao huku baadhi
wakitishia kumshitaki kwa kuwatapeli kwani wamepoteza fedha nyingi
kwenye mpango huo wakidai hawajaona chochote.
Joyce Kiria(kushoto), akifanya mahojiano na mmoja wa wanawake katika kipindi chake cha Wanawake Live.
“Dada Joyce aliwashawishi marafiki zake wengi, wakaingia na kila watu
walipomshtua na kumwambia kuwa ni utapeli mtupu alikuwa akiwatolea
lugha za kuudhi. Baada ya kunyetishiwa ‘ubuyu’ huo, Ijumaa Wikienda
lilimtafuta Joyce na kumuuliza juu ya ishu hiyo ambapo alifunguka: “Ni
kweli niliwashawishi marafiki zangu kwa sababu nilijua biashara hiyo
inalipa na hata mimi nimeumia sana kuona imekufa kwani sikupenda.
“Nimepoteza fedha nyingi. Ilikuwa ni kama desi ilivyokufa, hakuna wa kulaumiwa.”
Joyce aliongeza kwamba, kama kuna watu ambao wanadai amewatapeli waende mahakamani kwa sababu hakuwalazimisha kuingia wala hakuwashikia panga.
Joyce aliongeza kwamba, kama kuna watu ambao wanadai amewatapeli waende mahakamani kwa sababu hakuwalazimisha kuingia wala hakuwashikia panga.
Telexfree Network Marketing ni kampuni iliyokuwa ikijihusisha na
biashara ya mtandao ambapo mhusika hutoa kiasi cha fedha huku
akiunganisha watu wengine ambapo kipato chake kwa maana ya faida
itaongezeka mara kwa mara kwa kadiri anavyounganisha watu wengi.
No comments:
Post a Comment