Thursday, 6 November 2014

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA NUSU WAFAULU


Wanafunzi wa Shule ya Msingi Peaceland ya mkoani Mwanza wakishangilia baada ya kupata taarifa ya shule yao  kushika nafasi ya tatu kitaifa katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba wa mwaka 2014 yaliyotangazwa jana...

Dar es Salaam. Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), limetangaza matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka 2014 yakionyesha kuwa zaidi ya nusu ya wanafunzi waliofanya mtihani huo Septemba mwaka huu, wamefaulu.
Matokeo hayo yaliyotangazwa jana na Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde yanaonyesha kuwa wasichana wamefanya vizuri zaidi ya wavulana, huku ufaulu kwa jumla ukiwa umeongezeka kwa asilimia 6.38 ikilinganishwa na mwaka 2013.
Katika matokeo hayo Shule ya Twibhoki iliyopo mkoani Mara iliibuka ya kwanza kitaifa kati ya shule 15,867 zilizofanya mtihani huo ikifuatiwa na Mugini, Peacland na Alliance zote za mkoani Mwanza.
Shule ya tano ni Kwema ya Shinyanga ikifuatiwa na St Severine ya Kagera, Rocken Hill ya Shinyanga, Tusiime ya Dar es Salaam, Imani ya Kilimanjaro na iliyoshika nafasi ya 10 ni Palikas ya Shinyanga.
Wakuu wa shule vinara wazungumza
Mkuu wa Shule Twibhoki iliyopo Mugumu - Serengeti, Alphonce Magori alisema siri ya mafanikio hayo ni kila mwalimu kutambua nafasi yake.
Akizungumza ofisini kwake muda mfupi baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo alisema: “Kwanza ni mapenzi ya Mungu na uongozi wa shule kutambua nafasi ya kila mtumishi na wajibu wake na tunapata muda wa kujitathmini kama malengo yanafikiwa,” alisema.
Alisema wanafunzi nao hupata nafasi ya kutoa tathmini ya kile wanachofundishwa na wanapewa mazoezi ya mara kwa mara ambayo husaidia kujua uwezo wao na namna ya kuwasaidia.
Mwaka 2008 na 2010 ilikuwa ya pili kitaifa na tangu mwaka 2007 imekuwa ikiongoza kiwilaya na kimkoa.
Mkurugenzi wa Shule ya Alliance iliyoshika nafasi ya nne, James Bwire alisema baada ya mwaka jana kushika nafasi ya 15 waliweka mikakati. Alisema siri ya mafanikio hayo ni ushirikiano wa wazazi, walimu kujituma, mazingira mazuri ya shule na Ofisi ya Ukaguzi wa Shule Wilaya ya Nyamagana.
Meneja wa Shule ya Peacland ya Ukerewe ambayo mwaka jana ilikuwa ya 23, Halima Salum alisema alitarajia kupata mafanikio hayo kutokana na ufahamu wa wanafunzi waliomaliza mwaka huu.
Mchanganuo

No comments:

Post a Comment