Nabii Yaspi akiibariki moja ya pafyumu hizo.....
Hapa akiwapulizia wagonjwa mbalimbali.
NABII wa Kanisa la The Revelation Church lililopo
Buza-Kipera jijini Dar,Yaspi Paul Bendera, amefanya miujiza ya aina yake
kwa kuwatibu watu kwa kutumia pafyumu ambapo watu wenye magonjwa
mbalimbali walidai kupona kwa kupuliziwa pafyumu hizo.
Tukio hilo lilijiri Jumapili ya Novemba 2 mwaka huu ambapo kwa mujibu
wa Nabii Yaspi aliwaagiza wagonjwa wafike kanisani hapo na pafyumu
kanisani hapo ili azibariki na kuwa dawa na kinga yao kwa magonjwa
mbalimbali yanayowakabili.
Waandishi wetu waliokuwa kanisani hapo walishuhudia umati wa wagonjwa
wakiwa wamejipanga na pafyumu za kila aina na kuombewa kisha
kunyunyiziwa marashi hayo na kudai kupona kabisa.
No comments:
Post a Comment