DOA ndoano! Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline
Steven Pentzel ‘Jack Pentzel’ na mumewe Gardner Dibibi wanadaiwa
kukinukisha na kuingia kwenye gogoro la kila siku hadi mwanaume kutaka
kuondoka nyumbani wanakoishi Mbezi-Shamba jijini Dar...
Kikizungumza na Ijumaa Wikienda, chanzo makini ambacho ni mtu wa
karibu wa wanandoa hao, kilisema kwamba, kila kukicha wawili hao
wamekuwa wakigombana na sababu kubwa ni Jack kuchelewa kurudi nyumbani.
Ilidaiwa kwamba, tangu Jack awe na ushosti na staa mwenzake wa sinema
za Kibongo, Rose Ndauka amekuwa ni mtu wa kujiachia na kujisahau kwamba
ni mke wa mtu. “Yaani ndoa ya Jack inashikiliwa na uzi kwani kila siku
wanapigana na hivi karibuni mumewe alikusanya nguo na kuweka kwenye begi
akitaka kuondoka nyumbani.
“Tatizo mwanamke anachelewa kurudi nyumbani, mumewe akimuuliza ndiyo
mgogoro unaanzia hapo,” kilisema chanzo hicho. Baada ya kunyetishiwa
‘ubuyu’ huo, Ijumaa Wikienda lilimsaka mume wa Jack, Dibibi ili kueleza ukweli juu ya suala hilo.
‘Jack Pentzel’ na mumewe wakiwa kwenye picha ya pamoja na Rose Ndauka.
“Kutofautiana ni jambo la kawaida na huwa tunagombana tu kawaida
lakini siyo ugomvi mkubwa kama watu wanavyosema. “Sijaondoka nyumbani,
mbona nipo tu na mke wangu, hao wanaosema hivyo wanataka kutukosanisha
tu.”
Kumekuwa na uvumi wa kuvunjika kwa ndoa hiyo iliyofungwa mwanzoni mwa mwaka jana ambayo haijajaliwa kupata mtoto.
No comments:
Post a Comment