Friday, 31 October 2014

MFALME YA MWANA FA YAYIKISA

 
UKIACHILIA mbali ujio wake wa sasa,Kiboko Yangu alioshirikiana na Ally Saleh Kiba ‘Ally Kiba,’ mkongwe wa Bongo Fleva, Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ bado anatikisa na ngoma yake ya Mfalme....

Mkongwe wa Bongo Fleva, Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ akipanda jukwaani kutoa shoo.
Mfalme imetokea kuteka rika zote, ukiusikiliza kwa makini una ujumbe mzito ambao umekaa kimafumbo. Makala haya yanachambua mstari kwa mstari iliyopo kwenye ngoma hiyo kama ilivyofafanuliwa na MwanaFA mwenyewe:
Ilikuwaje ukapata idea ya kutengeneza Mfalme?
Awali kabisa nyimbo ilikuwa haiitwi Mfalme, wazo langu lilikuwa kutengeneza ngoma inayoitwa Sio Mimi ni Mungu lakini ilikuwa ikisema yote yale kwamba mie siyo maskini sana, nashukuru kwa nilichokipata japo yote si kwa uwezo wangu bali Mwenyezi Mungu. Alipokuja G. Nako tukashauriana tuiite Mfalme kutokana na mistari iliyopo.
Kanipa maarifa loloo
Yakanipa nyadhifa loloo
Kaziba nyufa loloo
Uwezo wa akili zangu wa kutambua kitu kizuri na kibaya na kupata nafasi ambazo nimezipata.
Sinung’uniki sina viatu wenzangu hawana miguu
Hawalalamiki wanamshukuru aliyejuu
Siwezi nikamletea makuu maombi ya kibraza du
Mbwembwe za kuomba magari nawaachia son I’m cool
Inawezekana nina matatizo, ili nifanye kizuri inabidi kuwafikiria walioko chini yangu na siyo kuwaangalia wa juu yangu. Kama unajiona una matatizo jua kuna wengine wanayo zaidi yako. Ni lugha ya picha mfano yule aliyepanga Tandale anawaonea wivu wa Masaki lakini kuna wengine hata hiyo ya Tandale hawana.
 ‘Mwana FA’ akikamua stejini.
Kama kipande cha kwanza cha mbao kwenye safina
Mimi ni kitu cha Mungu nafanya alichonituma
Kanipa ubongo una misuli na roho ya kitajiri
Sina kitu ila sina roho mbaya tunaishi vizuri
Wakati Nuhu kwenye kitabu cha maandiko alipopewa amri atengeneze safina alianza kuijenga mwenyewe. Safina ilikuwa ikitumika kuwaokoa watu kutoka kwenye gharika na kuwapeleka sehemu salama. Kwahiyo mimi ni kama kipande cha mbao nimetumwa kuwachukuwa watu (mashabiki) kuwapeleka sehemu salama.
Fukara nayeshukuru au tajiri nisiyekufuru
Najua bata najua hustle mi ni njiwa na kunguru
Wakati mwingine binadamu ukipata sana una uwezekano mkubwa wa kukufuru au ukikosa sana una kufuru sana na kuona kama Mungu amekuonea. Mie nipo katikati kama nikipata nashukuru Mungu na nikikosa nashukuru kwani najua kuna ambao hawana.
Naishi kwa mapenzi yake hakuna kitu naona hatari
Unapata ulichoandikiwa
Mungu hakupi kama hataki
Hata ukipora itapotea ili mradi yatimie maandishi
Kwenye dini kuna kudra. Mungu anakuwa amepanga wewe utapata hiki wewe hiki. Unaweza kufanya jitihada na isifikie mahali unataka iwe, ukiona hivyo ujue Mungu hakuwahi kukupa kama hataki jua mpaka
maandish yake yatimie.
Mkali ‘Mwana FA’ akipata sapoti ya kutumbuiza kutoka kwa 'linah'.
Mi ndo Vito wa Kolioni vitu vinaisha my way
Nife nikiwa muumini na everthing gon’ be I man
Vito Kolioni ni kiongozi mkuu kwenye filamu ya The Godfather. Alikuwa mkuu wa familia ya kimafia. Alikuwa akijaribu kubalansi kati ya mapenzi yake kwa familia yake na mapenzi ya Mungu. Alikuwa na nguvu nyingi na aliipenda familia yake, aliabudu na kuhangaika kwake kimaisha kunaenda kama alivyokuwa amepanga. Mwisho wa siku vyote vinaisha Mungu akiwa amepanga. Napenda nife nikiwa na muamini Mungu.
Najua anamipango, anafungua milango
Ndo anatoa michongo, namwita Mfalme wa Jungle
Huwezi kupewa mitihani isiyo na majibu. Kila ninachofikiria yeye ndiye anayetoa, kila kitu nilichokipata nimepata kwake.
Boss wa dunia yangu kanipa nguvu na ubongo
Mwenye maamuzi ya mwisho angetaka angeniumba Fungo
Mungu ameumba sisimizi, ameumba tumbili. Kama angetaka kukuumba vyovyote angeweza yote ni kwa maamuzi yake.
Mafala wana midomo ka vicheche usiwe kati yao
Wanaosema wenzao rudi angalia maisha yao
Wengine hawana hata kalaki wanaita watu maskini
Haki nawaombea mabaya kama wanavyoniombea mimi
Katika matumizi ya mitandao kila mtu ana maoni kuhusu chochote. Wengine wanapenda kuwanyooshea wenzao vidole hawajiangalii vinavyobakia kwao. Wana midomo kama vicheche (wanawake malaya). Wanashindwa kupima ni kama upande mmoja wamefungwa macho upande mwingine wamefunguliwa.
 
‘Mwana FA’ akicheza bila kukunja goti.
Na hata mtoa wa roho ni malaika, na nahisi ataenda peponi
Acha kuhukumu siyo kazi yako, we ni mwenzangu na mimi
Na una dhambi kama mimi, na hatujui kubwa za nani
Labda zako labda zangu, sio kazi yetu ni ya Maanani
Wakati unakufa kuna malaika anakuja kutoa roho yako. Pamoja na kuona kwamba anaua hutakiwi kumsema kwani ametumwa na anafanya kazi ya Mwenyezi Mungu. Yeye mwenyewe ni malaika na kazi yake ni malaika mtoa roho hivyo na yeye mwenyewe mwishoni ataenda peponi. Huna sababu ya kuhukumu watu acha waishi kwa maisha yao.
Usiniwaze sana mi nawaza maisha yangu
Sina hata mia ya urithi vyote hivi ni vya kwangu
Unatakiwa kujali sana maisha yako, kuna watu hawana hata kidogo na wanaishi vizuri, hawakurithi hata mia na wanaweza maisha yao wanayafanya na kuna waliorithi kila kitu na wameshindwa maisha yao.
Nshaenda shule bila viatu, nshatoa funza kama buku
Na ipo siku utaniheshimu ama utaheshimu hela zangu
Matatizo niliyopitia najiona tajiri japokuwa sijafika. Nishawahi kwenda shule bila viatu, nishawahi kutoa funza. Saa hivi vyote vinavyonitokea naviona starehe. Vingetokea wakati huo naenda shule na funza ningejiona bilionea wa ajabu.
Kwa mara nyingine, MwanaFA leo anakaribishwa nyumbani kwao Tanga ambapo atapiga bonge moja la shoo linalotambulika kama Vodacom Life is Better ndani ya Klabu ya La Casachika.

No comments:

Post a Comment