Mshambuliaji wa Yanga, Jerry....
Tegete
KIPA wa Stand
United, John Lwenda, amesema kuwa mshambuliaji wa Yanga, Jerry Tegete
alikuwa akihaha kutafuta bao kwa kupiga mashuti makali langoni mwake
kiasi kwamba alihisi anataka kumtoa uhai.
Kauli hiyo imekuja baada ya Yanga kushinda mabao 3-0 dhidi ya Stand,
kwenye Uwanja wa Kambarage, wikiendi iliyopita ambapo Tegete alifunga
mabao mawili huku Geilson Santos ‘Jaja’ akifunga moja.
Kipa huyo ameliambia gazeti hili kuwa, Tegete ni straika anayejua
jinsi ya kujipanga na kudai kuwa licha ya kuingia kipindi cha pili
katika mechi hiyo, makeke yake yalikuwa hatari na alikuwa akipiga
mashuti kila mara.
“Tegete sijui alitaka kuniua! Maana alikuwa akipiga mashuti makali
kila alipopata. Si kwamba mabeki walishindwa kumkaba ipasavyo, hapana,
ila jamaa anajua,” alisema kipa huyo.
No comments:
Post a Comment