
KUFUATIA kifo cha Rais Michael Chilufya Sata, kilichotokea tarehe 28
Oktoba 2014, mjini London na kwa kuzingatia Katiba yake Kifungu cha 38
(1) kinachohusu mamlaka ya Rais, kwamba nafasi ya Rais ikiwa wazi kwa
sababu yoyote ile, Makamu wa Rais atakaimu madaraka ya kiti cha Urais
hadi uchaguzi mdogo utakapofanyika ndani ya siku tisini (90), hivyo
Serikali imemteua Mhe. Guy Scott (MB), Makamu wa Rais, kukaimu nafasi
hiyo katika kipindi hiki cha mpito.
Tayari aliyekuwa anakaimu madaraka ya Urais, Mhe. Edgar Lungu (MB) ameshamkabidhi madaraka hayo.
Hadi sasa kulingana na taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, bado
haijafahamika maombolezo rasmi yataanza lini na kwa siku ngapi au
mazishi yatafanyika lini.
Haya yote yanategemea maamuzi ya kikao cha Baraza la Mawaziri ambacho kinakutana hivi sasa.
Hizi ni taarifa tunazoendelea kupokea, hivyo nasi tutaendelea kuwataarifu kwa kadri tunavyozipata.
No comments:
Post a Comment