Mshambuliaji Mrundi, Amissi Tambwe.
SIKU
chache baada ya kusaini mkataba wa kuitumikia Yanga, mshambuliaji
Mrundi, Amissi....
Tambwe, amekuwa akipokea simu nyingi za vitisho kutoka
kwa wadau wakimtisha juu ya uamuzi wake huo.
Tambwe alisaini mkataba wa mwaka mmoja Jumatatu iliyopita saa mbili
usiku mara baada ya uongozi wa Simba kumkabidhi barua ya kusitisha
mkataba wake, muda mfupi kabla ya kufungwa kwa dirisha dogo usiku wa
siku hiyo.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Tambwe alisema kuwa alianza kupigiwa
simu hizo muda mfupi baada ya kutangazwa kuwa anatua Jangwani ambapo
wengi waliompigia simu walijitambulisha kuwa ni mashabiki wa Simba na
kudai kuwa siyo wote waliomtishia bali wapo wengine waliompongeza.
“Unajua ninawashangaa mashabiki wa Simba hao ambao wananitisha, mimi
niliachwa na sikuondoka Simba mwenyewe kama wanavyofanya wachezaji
wengine, sasa wananipigia kunitisha ili iweje?
“Wengine wanasema kuwa nitajuta kuichezea Yanga, kitu ambacho siyo
sahihi, mimi kazi yangu ni soka, sasa iweje niache kusaini Yanga nikiwa
nimekatwa kwenye orodha ya wachezaji watakaoichezea Simba?
“Siyo sawa kabisa, wapo baadhi yao ni waelewa, wenyewe wananipigia na wengine kunitumia SMS za kunitakia kheri baada ya kusaini Yanga na kuniambia maishani popote kwa sababu wanaelewa sijaondoka mwenyewe, viongozi ndiyo walinikata katika usajili wao,” alisema Tambwe kwa masikitiko.
“Siyo sawa kabisa, wapo baadhi yao ni waelewa, wenyewe wananipigia na wengine kunitumia SMS za kunitakia kheri baada ya kusaini Yanga na kuniambia maishani popote kwa sababu wanaelewa sijaondoka mwenyewe, viongozi ndiyo walinikata katika usajili wao,” alisema Tambwe kwa masikitiko.
Wakati huohuo, Tambwe na kiungo Pierre Kwizera ambao wote
walisitishiwa mikataba yao kuitumikia Simba, wiki hii wanaendelea kusota
kufuatilia malipo yao ya kuvunjwa kwa mikataba hiyo huku kukiwa na
kauli tata kutoka pande zote mbili.
Akizungumzia juu ya malipo yake ya kuvunjwa kwa mkataba uliokuwa
umebakiza miezi sita, kati yake na Simba, jana mchana Tambwe alisema:
“Ninataka nimalizane na Simba kila kitu, ili niwe na amani ya kuitumikia
Yanga, bado hawajatulipa mimi na Kwizera.”
Naye Kwizera alisema: “Nimeshindwa kurejea nyumbani kwa kuwa bado
sijalipwa fedha za kuvunjwa kwa mkataba wangu ambao ulikuwa umebakiza
muda wa mwaka mmoja na nusu, niponipo tu kwa sasa naishi Sinza kwa
Tambwe.”
Gazeti hili lilipomtafuta Katibu Mkuu wa Simba, Stephene Ally na
kumuuliza juu ya suala hilo, jana mchana, alisema: “Tambwe na Kwizera
tayari tumemalizana nao kila kitu, ikiwemo barua ya kusitisha mikataba
yao na fedha zao wanazoidai Simba.”
Alipoulizwa Ofisa Habari wa Simba, Humphrey Nyasio, alisema:
“Wameshalipwa bana, waulize wao vizuri wanajua kila kitu.”Tambwe kwa
sasa amehamia Sinza kwa mdogo wake aliyekuwa akiishi naye awali, ametoka
Boko ambapo alikuwa akiishi kwenye nyumba aliyopangiwa na Simba.
No comments:
Post a Comment