
SIMANZI! Mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Abdu Jumaa iliyopo Kitunda, jijini Dar es Salaam, Enock Mseti (20) alitekwa na watu wasiojulikana kisha kuuawa kikatili na maiti yake kutupwa kando ya reli hivi karibuni....
Mwili wa Enock Mseti ukiandaliwa kwa ajili ya mazishi.
Akizungumza na mwandishi wetu nyumbani kwake Kitunda, baba mzazi wa
marehemu, Reuben Mseti alisema kijana wake ambaye hakuwa na tabia ya
kushiriki katika makundi maovu, aliondoka jioni baada ya kufanya kazi
zake za nyumbani kama ilivyokuwa kawaida yake.
“Mwanangu alikuwa afanye mtihani wa kidato
cha nne mwaka huu, ingawa kutokana na hali yangu kiuchumi kuwa mbaya,
alikuwa amesimama kwenda shuleni, lakini nilikuwa katika jitihada za
kuhakikisha anafanya mtihani huo,” alisema mzee Mseti kwa huzuni.
Jeneza likipelekwa makabulini kwa ajili ya mazishi.
“Hili ni pigo kubwa sana kwangu na familia yangu ndugu mwandishi,
maana kijana huyu ndiye alikuwa kila kitu hapa nyumbani, ukizingatia
mimi na mke wangu umri umeshatuacha. “Kwa jinsi mwili wake ulivyokutwa,
inaonekana aliuawa mbali na pale alipotupwa kwa sababu katika paji la
uso wake, kulionekana alama ya kupigwa na kitu kizito, mikono na miguu
yake ilikuwa imevunjwa, lakini nguo alizovaa hazikuwa na damu kuonyesha
kama kulikuwa na purukushani.
“Sehemu
aliyokutwa marehemu ni mita chache tu kutoka nyumbani katika eneo
ambalo lina kipori kidogo karibu na ilipopita reli,” alisema mzee Mseti.
Kijana ambaye ni msaidizi wa kazi za nyumbani kwa mzee huyo
aliyejitambulisha kwa jina la Seleman Abdallah alisema siku ya tukio
marehemu aliondoka na kurudi nyumbani majira ya saa nne kuulizia
chakula, akidai kuwa awekewe kidogo tu kwani asingekula sana, kisha
akaondoka.
“Marehemua aliondoka na akarudi kama saa 5 hivi usiku na kuondoka
tena, lakini safari hii hakurudi hadi tulipopata taarifa za kufa kwake
jambo ambalo lilitushangaza,” alisema Abdallah. Marehemu alizikwa katika
Makaburi ya Kinyamkera yaliyopo Kitunda jijini Dar es Salaam.
Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi, Amina.
Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi, Amina.
No comments:
Post a Comment