
Viongozi wa vuguvugu la
Katiba ya Wananchi, (UKAWA), wakionyesha hati ya makubaliano baada ya
kutia saini Jumanne Novemba 4, 2014 kwenye ofisi za makao makuu ya CUF,
Buguruni jijini Dar es Salaam... Chini ya makubaliano hayo, yaliyohusisha
vyama vinne, CHADEMA, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD, yataanza kutekelezwa
kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika baadaye
mwaka huu ambapo, UKAWA utamsimamisha mgombea anayekubalika kwenye eneo
husika bila ya kujali chama. Hata hivyo mwakilishi wa NLD hakuwepo na
ikaelezwa kuwa atasaini baadaye.

Sehemu yamakubaliano ya UKAWA yaliyotiwa saini.

Mwenyekiti mwenza wa UKAWA, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, akizungumza kuhusu ushirikiano huo.

Katibu Mkuu wa UKAWA, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Wilbroad Slaa, akizungumza kwa kutumia nyaraka.

Baadhi ya viongozi wa
UKAWA, wakielekea kwenye ukumbi wa mkutano makao makuu ya CUF, Buguruni
jijini Dar es Salaam, Jumanne Nov 4, 2014.

Kutoka kushoto, Katibu
Mkuu CHADEMA, Dkt. Wilbroad Slaa, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim
Lipumba, na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, wakisaini
makubaliano hayo ya UKAWA.

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, (Kulia), akizungumza baada ya kutiliana saini makubaliano hayo.
No comments:
Post a Comment