Waziri Mizengo Pinda.
“Ripoti inaweza kuiangusha Serikali kwa Waziri Mkuu
kulazimishwa kujiuzulu. Iwapo ripoti ya CAG itaonyesha kuwa suala hilo
siyo safi, basi Waziri Mkuu atatakiwa kujiuzulu kwa kuwa aliwahi kusema
suala la Escrow liko sawa,” alisema Zitto
Dodoma. Ripoti ya ufisadi katika akaunti ya Escrow itawasilishwa bungeni Novemba 27, mwaka huu na kujadiliwa baada ya Kamati ya Uongozi ya Bunge kuridhia kwamba Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) inaweza kushughulikia suala hiloTaarifa zinaeleza kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya baadhi ya wenyeviti wa kamati za Bunge ambao ni wajumbe wa Kamati ya Uongozi kutaka suala hilo lijadiliwe katika Bunge linaloendelea ili wanaopaswa kuwajibika kutokana na ufisadi huo wachukuliwe hatua.Mjumbe mmoja wa kamati ya uongozi ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema jana wamekubaliana kwamba hakuna haja ya kuundwa tume kama ilivyokuwa imeombwa awali na Mbunge wa Kigoma Mjini (CCM), Peter Serukamba bali, PAC ambayo ndiyo kamati husika inayoweza kuchunguza suala hilo na kuliwasilisha baada ya kupata ripoti ya Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

“Ripoti inaweza kuiangusha Serikali kwa Waziri
Mkuu kulazimishwa kujiuzulu. Iwapo ripoti ya CAG itaonyesha kuwa suala
hilo siyo safi, basi Waziri Mkuu atatakiwa kujiuzulu kwa kuwa aliwahi
kusema suala la Escrow liko sawa,” alisema Zitto.
Suala hilo lilizua mjadala bungeni juzi ambako
Ndugai akitoa mwongozo ulioombwa na Kafulila kwamba hoja hiyo kuhusu
lini Waziri Mkuu, Mizengo Pinda atawasilisha ripoti hiyo baada ya
uchunguzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na CAG
kukamilika kwa kuwa ni ya haraka alisema; “Suala la Kafulila
tutalishughulikia kwenye Kamati ya Uongozi kwa kuwa kiti hiki hakina
mamlaka.”
Baada ya Kafulila kuomba mwongozo huo aliungwa
mkono na wabunge wa upinzani na baadaye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi alisimama na kusema, “Ni
kweli Waziri Mkuu alitoa maelekezo kwa Takukuru na CAG kufanya uchunguzi
huo na kukabidhi ripoti kwake ili atoe taarifa bungeni, lakini kazi
hiyo haijakamilika.”
Lukuvi alisema ukaguzi wa CAG bado unaendelea kwa
kuwa unahusu mambo mengi na kwamba taarifa zinaeleza kuwa wako mbioni
kukamilisha hivyo wakikabidhi kwa waziri mkuu itawasilishwa bungeni na
kukabidhiwa kwa Spika kwa ajili ya utekelezaji.
Alisema taarifa hizo mbili hazijakabidhiwa kwake
na kwamba Takukuru ikimaliza uchunguzi wake inaweza kuchukua hatua
yenyewe lakini taarifa inayosubiriwa na Bunge ni ya CAG.
No comments:
Post a Comment