Wednesday, 5 November 2014

KALAMA: ISABELA NI MSALABA WANGU

MKONGWE wa Bongo Fleva na mwanachama wa kundi la Gangwe Mob, Luteni Karama ambaye ni mchumba wa aliyekuwa Miss Ruvuma miaka ya nyuma, Isabela Mpanda, amekiri kuwa bibie huyo ni msalaba wake, hivyo hata amkosee kiasi gani, hatamuacha.....

Aliyekuwa Miss Ruvuma miaka ya nyuma, Isabela Mpanda akipozi.
“Mimi nimeshakubali kuwa Bela ni msalaba wangu na ndiyo maana hata kama ananikosea vipi au mimi namkosea, tunaweka mambo sawa na maisha yanaendelea kama kawaida,” alisema Karama ambaye mshirika wake, Inspekta Haroun, juzikati aliadhimisha miaka kumi ya ndoa yake.
Mkongwe wa Bongo Fleva na mwanachama wa kundi la Gangwe Mob, Luteni Karama.
Maisha ya wawili hao kimapenzi yamekuwa ya kutatanisha hasa kutokana na kuachana na kurudiana kila mara, kitu ambacho Karama anasema kitafikia mwisho kwani furaha yake ni kuona anafunga ndoa na mpenzi wake huyo wa muda mrefu.

No comments:

Post a Comment