Mada
iliyopo mezani ni faida na hasara za wapendao kufanya kazi ofisi moja
ambayo tulianza kuijadili wiki iliyopita. Uhali gani msomaji wangu? Ni
matumaini yangu kwamba unaendelea vizuri na majukumu ya ujenzi wa taifa.
Karibu tena kwenye busati letu ambapo tunajuzana mambo mbalimbali
yahusuyo mapennzi.....

Wiki
iliyopita, tulijadili changamoto mbalimbali wanazokutana nazo wanandoa
au wawili wapendanao wanaofanya kazi kwenye ofisi moja na mwisho,
niliishia kukueleza nini kifanyike ili kuzuia matatizo yanayoweza
kujitokeza.
NINI CHA KUFANYA?
Matatizo katika sehemu za kazi, hasa kwa wapendanao yapo na hayakwepeki lakini ukizingatia yafuatayo, utaishi vizuri na mwenzi wako, uhusiano wenu wa kimapenzi utaimarika na ufanisi kazini utaongezeka pia.
Matatizo katika sehemu za kazi, hasa kwa wapendanao yapo na hayakwepeki lakini ukizingatia yafuatayo, utaishi vizuri na mwenzi wako, uhusiano wenu wa kimapenzi utaimarika na ufanisi kazini utaongezeka pia.
1. USICHANGANYE MAPENZI NA KAZI
Yawezekana usiku kucha wewe na mwenzi wako hamkulala, mmekesha
mkipigana, kurushiana maneno makali au mlilala mzungu wa nne. Hata
hivyo, unapaswa kujua kwamba ukifika kazini, mambo yote ya usiku
unayaacha nyumbani na unamchukulia mwenzako kama mfanyakazi mwenzako wa
kawaida.
Huna haja ya kununa, kuwa na kisirani au kuharibu kazi kwa sababu jana uligombana naye. Fanya kazi na muda wa kurudi nyumbani ukifika, kaendeleeni na migogoro yenu. Ni makosa makubwa kuhamishia matatizo ya nyumbani kazini.
Huna haja ya kununa, kuwa na kisirani au kuharibu kazi kwa sababu jana uligombana naye. Fanya kazi na muda wa kurudi nyumbani ukifika, kaendeleeni na migogoro yenu. Ni makosa makubwa kuhamishia matatizo ya nyumbani kazini.
Pia kama umekosana na mwenzi wako kazini kwa sababu za kikazi, huna
haja ya kuendelea kununa hadi nyumbani, utakuwa unahatarisha uhusiano
wako. Lazima kuwe na mipaka kati ya mambo ya kifamilia na mambo ya
kizazi.
2. MWACHE AWE HURU
Haina maana kwamba kwa sababu ni mkeo, mumeo au mpenzi wako, basi
hana haki ya kuzungumza au kucheka na watu wengine isipokuwa wewe tu.
Mpe uhuru, hata kama anachanganyikana na watu wa jinsia tofauti, huna
haja ya kukasirika au kujisikia wivu. Mwache abadilishane mawazo na watu
wengine na akija kwako, atakuwa mpya kabisa.
Acha kumganda, siyo lazima kila mara aende na wewe ‘lanchi’, nafasi
yako ni nyumbani lakini kazini kila mmoja anao uhuru wa kuchanganyikana
na marafiki na wafanyakazi wenzake.3. USIINGILIE MAMBO YAKE BINAFSI
Yawezekana mumeo, mkeo au mpenzi wako amekorofishana na mfanyakazi
mwenzake kwa sababu za kikazi au nyinginezo, hayo ni mambo ya kawaida
katika sehemu za kazi. Acha kuingilia ugomvi wake au kumtetea wakati
mwenyewe hajakuomba kufanya hivyo. Muache amalize matatizo yake mwenyewe
na hiyo itamfanya ajisikie huru zaidi. Kwa wanawake, kutongozwa sehemu
za kazi ni mambo ya kawaida hivyo usikasirike na kupandisha jazba
ukisikia kuna ‘njemba’ inammendea mwenzi wako.
Muamini na mpe nafasi ya kukabiliana na changamoto kama hizo kwani
kwa mwanamke anayejiheshimu, lazima akulindie heshima yako hata kama uko
mbali au hujui chochote.
4. KUWA NA NIDHAMU KAZINI
Ni vigumu kwa mtu anayejiheshimu, kukosewa adabu na wengine kwa
urahisi. Ukishajua unafanya kazi na mwenzi wako ofisi moja, jitahidi
kujiheshimu kwa kujiepusha na ubishi usio na msingi, masihara yaliyovuka
mipaka au ugomvi kwani ni rahisi kufanyiwa tukio baya kama kutukanwa,
kupigwa au kufanyiwa masihara mabaya mbele ya mwenzi wako, jambo ambalo
lazima litaziumiza hisia zake.
5. ONESHA BIDII YA KAZI
Miongoni mwa mambo yanayoweza kumfanya mtu akaheshimika kazini, ni
bidii na ufanisi katika kazi yake. Jitahidi kujielimisha kadiri uwezavyo
kuhusu kazi unayoifanya na kuwa na bidii kwani kila mtu atakupenda na
kukuheshimu.
Mwenzi wako pia atazidisha mapenzi kwako kwani atajisikia fahari
jinsi watu wengine wanavyokutolea mifano mizuri.Ni matumaini yangu kuwa
utakuwa umejifunza kitu, tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine.
No comments:
Post a Comment