Staa wa Bongo Movie,...
Esha Buheti.
STAA wa Bongo Movies, Esha Buheti amejiapiza kiapo
cha kifo kwa kusema kuwa kama ipo siku atajaribu mchezo wa usagaji basi
atakapomaliza tu litokee gari na kumkanyaga na kufa.
Akizungumza na mwandishi wetu, Esha alisema kuwa alishajiapiza kwa
kutumia Msahafu ya kuwa kamwe hawezi kufanya tendo hilo akiamini kuwa
liko kinyume kabisa na Mwenyezi Mungu. “Kwa kweli mimi nikifanya usagaji
siku hiyo nikimaliza tu wakati natoka basi lije gari tena kubwa na
kunigonga nife kabisa,” alisema Eshe.
Hivi karibuni vitendo vya kisagaji vimeshamiri kwa kasi huku mastaa wengi wa filamu wakitajwatajwa kujihusisha navyo.
No comments:
Post a Comment