Beki na nahodha wa Yanga,....
Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
BEKI na
nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ anatarajiwa kuikosa mechi
yenye upinzani mkubwa ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC.
Mechi hiyo ni muhimu kwa beki huyo kucheza kutokana na aina ya
washambuliaji wa Azam FC. Mtanange huo utapigwa Desemba 28, mwaka huu
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Cannavaro ataikosa mechi hiyo kutokana na kadi nyekundu ya moja kwa
moja aliyopewa kwenye mechi ya ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar iliyopigwa
kwenye Uwanja wa Kaitaba juzi. Kagera ilishinda 1-0.
Beki huyo, alipewa kadi hiyo baada ya kumpiga kichwa mshambuliaji wa Kagera Sugar, Rashidi Matalanda.
Kwa mujibu wa kanuni za soka, beki huyo anatarajiwa kukosa mechi mbili za ligi kuu ambazo ni dhidi ya Mgambo JKT itakayochezwa Jumamosi ijayo na Azam FC, zote zitachezwa Uwanja wa Taifa, Dar.
Kwa mujibu wa kanuni za soka, beki huyo anatarajiwa kukosa mechi mbili za ligi kuu ambazo ni dhidi ya Mgambo JKT itakayochezwa Jumamosi ijayo na Azam FC, zote zitachezwa Uwanja wa Taifa, Dar.
Adhabu hiyo, pia itampata kocha msaidizi wa timu hiyo Mbrazili,
Leonardo Neiva ambaye alitolewa kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja
kwenye benchi baada ya kuingia uwanjani dakika chache baada ya Cannavaro
kupewa kadi nyekundu.
Beki na kocha huyo wanatarajiwa kurejea uwanjani katika mchezo dhidi
ya Mbeya City utakaopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine Januari 3, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment