Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva.
BABA
wa kiungo mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva ambaye ni Happygod Msuva
ameeleza kushangazwa na taarifa kuwa Simba inataka kumsajili mtoto wake....
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Pope,
alinukuliwa akisema kuwa, baada ya kumsainisha mkataba mpya kiungo wao,
Jonas Mkude, sasa wanamhitaji Msuva.
Hans Pope alisema kuwa, dau la kuanzia kumsajili Msuva walilotenga ni
shilingi laki tano, hivyo wanajipanga kutuma maombi Yanga. Akizungumza
na Championi Ijumaa, Happygod alisema aliwahi kumpeleka mwanaye kwenye
timu hiyo lakini walimwekea pozi.
“Unakumbuka kipindi kile Simon alikuwa akizomewa mara kwa mara na
mashabiki wa Yanga? Basi nikaamua kwenda kuzungumza na aliyekuwa
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Rage na makamu wake, Geofrey Nyange
‘Kaburu’, walitoa majibu ya dharau kila nilipowapigia simu.
“Yanga imechangia kumlea Simon mpaka hapo alipo baada ya kuanzia
katika Academy ya Azam FC, nilipoona hakuna maendeleo wakati akiwa chini
ya Idd Cheche na Kali Ongala, nikampeleka Moro United ndipo Seif Magari
akamchukua na kumpeleka Yanga.
“Hivyo kama Simba wanamtaka, wawafuate Yanga kwa kuwa bado ana
mkataba, lakini ukweli ni kuwa ninawashangaa hao Simba wanamtaka Simon
kwa kipi!” alisema Happygod.
No comments:
Post a Comment