Pembe za ndovu.
SERIKALI ya Tanzania imeshtushwa na ripoti inayoelezea biashara
haramu ya pembe za ndovu kati ya baadhi ya viongozi wa nchi hiyo na
China....
Serikali hiyo imesema imesikitishwa na ripoti iliyotolewa na taasisi
ya uchunguzi ya mazingira inayodai kwamba majangili wa Kichina
wakishirikiana na baadhi ya viongozi wa serikali ya Tanzania ndio
wanaoangamiza idadi ya tembo kutokana na biashara haramu ya pembe za
ndovu.
Inadaiwa kwamba raia wa China walitumia ziara ya rais wao, Xi Jinping
ya nchini Tanzania kusafirisha kimagendo maelfu ya kilo za pembe za
ndovu.
Kulingana na shirika la utafiti wa mazingira, EIA, Pembe hizo zilinunuliwa wiki moja kabla ya ziara ya rais huyo nchini mwaka jana na zilifichwa katika mifuko ya wanadiplomasia ili zisitambuliwe.
Kulingana na shirika la utafiti wa mazingira, EIA, Pembe hizo zilinunuliwa wiki moja kabla ya ziara ya rais huyo nchini mwaka jana na zilifichwa katika mifuko ya wanadiplomasia ili zisitambuliwe.
Msemaji wa Serikali Assah Mwambene amemwambia mwandishi wa BBC
Aboubakar famau kwamba ripoti kama hiyo zinatatiza jitihada za serikali
kukabiliana na uuzaji haramu wa pembe za ndovu.
No comments:
Post a Comment