
KIBANO! Kuonesha wapo
‘serious’ na mavazi, polisi walimtaiti staa wa Bongo Fleva, Rashid
Makwiro ‘Chid Benz’ na kumtaka akavae vizuri kisha arejee mahakamani.
Tukio hilo lilitokea juzi, Jumanne katika...........
Makahama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar, wakati staa huyo alipokuwa amefikishwa kusomewa mashtaka yake ya kukutwa na madawa ya kulevya.
Makahama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar, wakati staa huyo alipokuwa amefikishwa kusomewa mashtaka yake ya kukutwa na madawa ya kulevya.
Staa wa Bongo Fleva, Rashid Makwiro ‘Chid Benz’ akiwa chini ya ulinzi mkali ndani ya Makahama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar.
Akiwa katika viunga hivyo vya mahakama,
Chid Benz alionekana akiwa ametinga jinzi ambayo ililegezwa mkanda na
alipoingia ndani ya chumba cha mahakama, mlegezo uliongezeka zaidi hadi
kufikia chini ya makalio kitendo ambacho polisi walishindwa kukivumilia.
Kuonesha kwamba hawakufurahishwa na kitendo hicho, maafande waliokuwa
wakimsindikiza Chid mahakamani hapo, walimtaiti kwa kumshika kiunoni na
kumtoa nje kwenda kumpandisha suruali hiyo kisha kumrudisha akiwa amevaa
vizuri.
Mwana Hip hop huyo, ‘Chid Benz’ akivaa kwa adabu zaidi.
Akiwa mahakamani hapo mbele ya Hakimu Waliarwande Lema na mwendesha
mashtaka, PP Mwanaamina Komba, Chid alisomewa mashtaka matatu alyokutwa
nayo Oktoba 24, mwaka huu katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere
jijini Dar. Mashtaka hayo ni; kukutwa na madawa ya kulevya aina ya
heroin gramu 0.25 yenye thamani ya Sh. 38,638, bangi gramu 1.72 ambayo
thamani yake ni Sh. 1,720 na vifaa vya kuvutia (kifuu cha nazi na
kijiko).
Chid aliyakana mashtaka yote matatu hakimu akaahirisha kesi hiyo hadi
Novemba 11, mwaka huu na kuweka dhamana wazi ya faini ya shilingi
milioni moja na wadhamini wawili lakini mshtakiwa hakukidhi masharti ya
dhamana, akaomba kukamilisha masharti hayo kesho yake (Jumatano) hivyo
akarudishwa mahabusu Segerea.
No comments:
Post a Comment