Rushwa ni miongoni mwa vichocheo vikubwa vya umaskini hapa nchini Tanzania.
Siyo kichocheo cha umaskini tu, bali pia ni kikwazo kikubwa cha maendeleo katika nchi ambazo shida hii imeshamiri na kuota mizizi.
Siyo kichocheo cha umaskini tu, bali pia ni kikwazo kikubwa cha maendeleo katika nchi ambazo shida hii imeshamiri na kuota mizizi.
Rushwa iliyokithiri katika nchi yoyote, huathiri utawala bora na
kushindwa hata kwa nguvu za soko kiuchumi katika nchi husika.Rushwa
iliyokithiri siyo tatizo linaloikumba Tanzania peke yake, bali dunia
nzima na ni tatizo kubwa sana linalokera jamii, kiasi cha kuhatarisha
utulivu na amani katika nchi mbalimbali duniani.
Takwimu zilizotokana na utafiti au tathmini iliyofanywa na taasisi ya
kimataifa ya Transparency International, yenye makao yake makuu nchini
Ujerumani mwaka 2013, inadhihirisha kuwa rushwa ni tatizo la dunia
nzima.
Watanzania watatakiwa waifahamu tafsiri sahihi ya rushwa kwani
haishii katika tendo la kutoa au kupokea hongo peke yake ili kurahisisha
zaidi upatikanaji wa huduma za kijamii bila bughudha.
Transparency International imeitafsiri rushwa kwa maneno haya
yafuatayo: Kwamba ni matumizi mabaya (ya madaraka katika ofisi au
taasisi ya umma) kwa manufaa au masilahi binafsi.
Katika tathmini ya viwango vya rushwa kimataifa ya mwaka 2013 ,
iliyofanywa na taasisi hiyo, Tanzania ilishika nafasi ya 111 miongoni
mwa nchi 117 duniani, yaani ni wa sita kutoka mkiani! Aibu kubwa hii!
Tathmini hiyo ilikuwa ni kwa kutumia kiashiria chao kinachoitwa ‘Corruption Perception Index’, ikilinganishwa na nafasi ya 88 miongoni mwa nchi 159 katika tathmini iliyofanyika mwaka 2005.
Tathmini hiyo ilikuwa ni kwa kutumia kiashiria chao kinachoitwa ‘Corruption Perception Index’, ikilinganishwa na nafasi ya 88 miongoni mwa nchi 159 katika tathmini iliyofanyika mwaka 2005.
Hii maana yake ni kwamba rushwa inazidi kukua na kuota mizizi katika
nchi yetu na hakika niseme wazi kwamba ni hatari kwa usalama wa nchi
yetu, vizazi vya sasa na vijavyo.Rushwa imeingia hata katika mikataba
mbalimbali ya nchi, tumeshasikia malalamiko kwenye sekta ya madini,
umeme, miundombinu na kadhalika.
Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere enzi za uhai
wake alikemea sana ‘mdudu’ rushwa, lakini inaonekana amepuuzwa kwani
mianya inaachwa bila kuzibwa.
Tunaelekea kwenye chaguzi mbalimbali kuanzia za viogozi wa serikali
ya mitaa au vitongoji na vijiji hadi kwenye udiwani, ubunge na baadaye
urais. Ni wakati mwingine wa rushwa kutawala katika jamii na nina hakika
tutashuhudia mengi.
Tutashuhudia wagombea wakimwaga fedha na kujifanya ni takrima kwa
wapiga kura na makundi yao na nina hakika baada ya chaguzi hizo
malalamiko mengi ya utoaji rushwa yatasikika karibu kona mbalimbali za
nchi yetu.
Tatizo hili la utoaji na upokeaji rushwa siyo la Tanzania peke yake,
bali Afrika Mashariki nzima na duniani kote. Lazima tujitathmini
wenyewe. Madhara ya mwenendo huu wa utoaji rushwa kwa vizazi vya sasa
upo hivi je, jamii ya vizazi vijavyo itakuwaje?
Hivi sasa kumejengeka kwamba mtu hawezi kupata huduma fulani mpaka
atoe rushwa hata kama ni haki yake.Tunaelekea wapi?Hakika, tumejiingiza
katika sakata la mambo ambayo hayakubaliki kimaadili duniani kote! Au
tumejisahau tulikotoka na hatujui tuendako?
Vijana wetu siku hizi wengi wanadhani na kuamini katika akili zao
kuwa bila kutoa rushwa huwezi kufanikiwa katika jambo lolote na hili
ndilo linasababisha hata mitihani kuibiwa na kusambaa kwa watahiniwa.
Vijana wa siku hizi wanaamini kuwa ili wapige hatua kimaendeleo basi
wapate kazi ambazo mianya ya rushwa ipo nje nje. Wanataka baada ya miaka
miwili kazini wawe na nyumba na gari la kisasa kutokana na kula rushwa!
Hiyo ndiyo jamii tunayoijenga. Hili ni bomu ambalo lipo mbele yetu.
Ukienda katika hospitali nyingi za umma, rushwa inawekwa mbele ili
utibiwe na hata ukitaka haki yako, baadhi ya watendaji watakuomba
rushwa.
Vyombo vya kulinda sheria kama mahakama na polisi, baadhi ya
watendaji wameonekana kwamba rushwa ni jambo la kawaida. Hata Tume ya
Jaji Warioba iliona hili, ikashauri lakini ikapuuzwa, hakuna
kilichofanyika kubana mianya hiyo.
Tukitaka kupiga hatua kimaendeleo safari hii mtu yeyote ambaye
ataomba uongozi wa kuchaguliwa, tukijua kuwa amekuwa akitoa rushwa,
atengwe na aogopwe kama ukoma.
No comments:
Post a Comment